IBIHUHA.COM

Friday, July 2, 2010

Mtoto abakwa hadi kufa

MTOTO mwenye umri wa miaka 10 aliyekuwa akisoma darasa la pili katika Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa amekufa baada ya kubakwa.

Watu wasiojulikana walimbaka mtoto huyo na kuutelekeza mwili wake.

Unyama huo ulitokea juzi katika kitongoji cha Bangwe, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa,
Isuto Mantage amethibitisha kutokea kwa unyama huo.

Kamanda Mantage amesema, Polisi wanawasaka waliohusika na mauaji hayo.

Kamanda Mantage alisema kabla ya tukio, mtoto huyo alimuaga mama yake (jina linahifadhiwa) kuwa anakwenda kumsalimia dada yake mkubwa anayeishi eneo lingine.

“Lakini mtoto huyo hakurudi nyumbani tena hali iliyomfanya mama yake aamini kuwa
ameamua kulala kwa dada yake kwani alikuwa na mazoea ya kufanya hivyo,” alisema Kamanda.

Baada ya kubaini kwamba mtoto huyo hakulala kwa dada yake, alitoa taarifa kwenye uongozi wa mtaa, wakaanza kumsaka na ndipo mwili ukakutwa kwenye jumba lisilokaliwa na watu huku mdomoni akiwa amezibwa kwa kitambaa.

Uchunguzi wa daktari umebainisha kuwa mtoto huyo kabla ya kifo chake alibakwa kwa
zamu na kusababisha kuvuja kwa damu nyingi.

No comments:

Post a Comment

tubabarire ubanze wiyandikishe rwose!